Posted by
KANGOZI OFFICIAL
on
- Get link
- X
- Other Apps
Arsene Wenger ameionesha dunia kwa mara nyingine kwamba yeye sio mtu wa mchezo mchezo baada ya leo kuipoteza Tottenham Hotspur na kuwapiga bao mbili kwa sifuri nyumbani kwao.
Halikuwa jambo la kushtua sana kwani tangu Marcio Pochettino ajiunge na Tottenham hajawahi kupata alama 3 kati mechi na Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Huu ulikuwa mchezo wa 10 kwa Arsenal kushinda mfululizo katika uwanja huo na hii ikiwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kushinda idadi kubwa ya mechi kiasi hicho katika uwanja huo.
Alikuwa ni Shkordani Mustafi dakika ya 36 kupeleka kilio kwa Tottenham Hotspur likiwa ni bao lake la kwanza katika uwanja wa Emirates kabla ya Alexis Sanchez kufunga bao la pili na la ushindi.
Mabao mawili ya leo ya Arsenal yanawafanya sasa kufunga mabao 250 zidi ya Tottenham Hotspur na yamewafanya kufikisha alama 22 na kukaa katika nafasi ya 5 ya Epl wakisikilizia matokeo ya mechi ya Liverpool.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments